Serikali yaahidi kuwapandisha vyeo wafanyakazi wake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi nyongeza ya kawaida kwa mishahara na kuwapandisha madaraja wafanyakazi wote wanaostahili.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo katika maadhimisho ya sherehe ya Mei Mosi,alipokuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Hata hivyo, Rais Magufuli alisema Serikali ilisitisha upandishaji wa vyeo na mishahara kutokana na kuwepo na watumishi hewa na walioghushi vyeti, lakini baada ya kuondolewa kwao, serikali itahakikisha inashughulikia maslahi ya wafanyakazi.
“Watumishi 9932 walikuwa na vyeti feki,watumishi hewa walikuwa 19706 hivyo kama Serikali ingeongeza mishahara inamaana watumishi hawa pia wangefaidika na pesa ambazo hawakustahili kuzipata,” alisema RaisMagufuli.
Aidha aliwataka waajiri kuheshimu na kutoa mikataba ya kazi na kutowanyanyasa wafanya kazi wao na wafanyakazi kuomba kazi kulingana na elimu zao na waache tabia ya kughushi vyeti.
Maadhimisho hayo yaLIhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai,Naibu Spika Tulia Ackson, Mawaziri Jenister Mhagama na Angella Kairuki, Profesa Jumanne Maghembe na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na baadhi ya Wabunge. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ilikua ni “Uchumi wa Viwanda Vizingatie Haki, Maslahi na Heshima ya Mfanyakazi”.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment