Shamsa Ford akanusha kumfilisi mume wake Chidi Mapenzi

Msanii wa filamu, Shamsa Ford amefunguka kukanusha taarifa ambazo zimezagaa katika mitandao kijamii kuwa amemfilisi mume wake, Chidi Mapenzi ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo

Shamsa Ford akiwa na mume wake Chidi Mapenzi
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni mfanyabishara huyo kufunga duka lake lililokuwa Vijana, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Shamsa amedai hatua hiyo imekuja baada ya Chidi Mapenzi kubadili mfumo wa maisha yake baada ya kuingia kwenye maisha ndoa.
“Kusema kweli taarifa za sijui kumfilisi mume wangu nimezisikia sana na nimeumia sana, kitua ambacho nataka mashabiki wangu wajue sio kweli huo ni uzushi tu,” alisema Shamsa. “Kilichotokea mume wangu kuna sehemu alifungua duka sasa bei ya kodi likuwa kubwa sana kuliko mauzo. Mimi nikashauriana na mume wangu kwanini tusihame hapa na tuhamie sehemu ambayo ina bei ya kawaida ambayo tunaweza kufanya biashara vizuri, ndipo tulipohamia sehemu nyingine lakini tunamshukuru mungu mambo yanaenda vizuri,”
Aliongeza, “Mimi nimeshazoea kusemwa vibaya naumia lakini ndio hivyo, mwisho wa siku watu waliozoea kumuona Chidi Mapenzi akitumbua, sijui akifanya nini sasa hivi ni mume wa mtu na ana majukumu. Kwahiyo kama hamjui mume wangu kamebadili style ya maisha yake lakini mambo yapo sawa,”
Katika hatua nyingine muigizaji huyo amewataka mashabiki wake wa filamu kukaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa filamu yake mpya akiwa na Gabo Zigamba.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment