Tunamtafuta Ben Pol atueleze kuhusu zile picha za nusu utupu – BASATA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA, Godfrey Mngereza amelaani picha za nusu za utupu za msanii wa muziki, Ben Pol ambazo imezua tafrani kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Godfrey Mngereza
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Mngereza amewataka wasanii kufanya kazi nzuri ambazo zinaweza kuwaweka sehemu nzuri na siyo kutengeneza mazingira ambayo yanautia dosari muziki wao.
“Sisi kama BASATA tumeona hizo picha mtandaoni, siyo kitu kizuri, kwanza hakiendani na tamaduni zetu. Kwahiyo sisi tunamtafuta Ben Pol halafu tumsikilize, atueleze zile picha ilikuwaje mpaka zikasambaa mitandaoni. Tukiongea naye tunaweza kutoa kauli yoyote na kulaani matukio ya namna hiyo,”
Aliongeza,” Pia naungana na wasanii waliolaani kitendo hiko ambacho ni cha ajabu sana na baraza kwa mamlaka yake kama mzazi haiwezi kukaa kimya lazima tujue kama ana tatizo la akili au maadili limemkumba Ben Pol.”
Pia Mngereza amewaomba wasanii wa Tanzania kwa upande wa muziki wafanye muziki mzuri wasitegemee kiki.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment