Wasanii waguswa na vifo 32, Arusha

Huzuni umetanda, Wilayani Karatu Arusha na Tanzania nzima baada ya kutokea ajali mbaya ya basi iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wagari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha.

Ajali hiyo imetokea Jumamosi hii saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria wanafunzi hao kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu mkoani humo.
Kufutia ajali hiyo, wasanii wa muziki na filamu wametoa salamu zao za rambirambi kwa ndugu, jamaa, marafiki pamoja na watu walioguswa na msiba huo.
Hizi ni salamu za pole za wasanii hao.
Diamond
Kwa niaba ya uongozi na team nzima ya @wcb_wasafi ningependa nitoe Pole kwa Familia zote ambazo watoto wao walikuwepo kwenye ajali hii….tupo nao pamoja katika kipindi hichi kigumu… Mwenyez Mungu awasaidie wapone haraka wote wenye majeraha na azilaze Roho za Marehem wote Mahali pema Pemponi Amin๐Ÿ™

Mwana FA
Hii habari ya Karatu inasikitisha sana,vitu vibaya ambavyo havipo ndani ya uwezo wetu kuvizuia..Mungu awasitiri na azipe nguvu familia zao‬!

Mansu Li
Mola watie nguvu wazazi/ndugu wa watoto waliyopoteza maisha kwenye ajali leo, na uwalaze pema marehemu In Shaa Allah ๐Ÿ™๐Ÿฟ ( Innah lillahi wa innah ilayhi raajiun )

Vanessa Mdee
Ni huzuni mkubwa kuamka na kupata taarifa ya ajali iliyo chukua roho za ndugu zetu huko Karatu..Mungu awape nguvu wanafamilia katika kipindi hichi kigumu. Mungu ndio mpangaji na tunaomba alaze roho za ndugu zetu waliopoteza maisha yao kwa ajali leo huko karatu.

Dogo Janja.
ole zangu za dhati ziwafikie familia zilizopoteza watoto wao kwenye ajali May their sweet souls rest in eternal peace. Amen

Nay wa Mitego
Daaaah.! Wanasema Hakuna aijuae Kesho yake. Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahara pema๐Ÿ™๐Ÿฟ. Pole kwa Familia zote zilizo patwa na Msiba huu๐Ÿ˜ญ

Shamsa Ford
Mungu una makusudi yako kwa haya yote hatuwezi kukulaumu ingawa inauma sana.Naomba uwatie nguvu wazazi wa hawa watoto..inauma sana jamani Mungu azipumzishe roho za watoto mahali pema peponi inshaallah..

AY
Mungu walaze Mahali Pema Peponi wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha yao kwenye ajali mbaya ya gari na uwajaalie familia zao nguvu katika kipindi hiki kigumu..Ameen ๐Ÿ™๐Ÿฟ
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment