Watakaowapa wanafunzi ujauzito kukiona cha moto

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, ametoka agizo kuwa ni marufuku kwa walimu na watu wazima watakaobainika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi na kuchukuliwa sheria bila kuonewa huruma.

Kauli hiyo ilitolewa wilayani Ukerewe na Mkuu wa Mkoa wa Mwaza, John Mongella wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wilayani humu.
Alionya kuwa ni marufuku kuunda tume ya kuwachunguza watuhumiwa walimu wenye matatizo ya aina hiyo kwa ngazi walizofikia kuwajaza wanafunzi ujauzito.
Sambamba na kuonya suala hilo, Mkuu wa mkoa alimwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe (OCD), Ignus Kapira kuwa uchunguzi wa kesi hizo usikuchukue zaidi ya wiki moja. “Ni marufuku kuunda tume ya kuchunguza watuhumiwa wa aina hiyo.Tatizo hili la mwalimu kwa ngazi uliyofikia unampa ujauzito mwanafunzi upate nini.”
Aliongeza Mongella kuwa “Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, OCD tena wewe tumekuleta hapa ni mpya kesi hizo za kubaka usimwachie mtu.Kama ni kiongozi,mwalimu ama mtu mzima,usimwachie mtu huyo nenda mahakamani kasimame naye mahakamani kama nako kuna tatizo nipigie simu tuhangaike naye huyo mtu.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment