Yeriko Nyerere akamatwa na watu wanaodhaniwa polisi

Mwanachama wa Chadema Yeriko Nyerere, anadaiwa kukamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi au usalama wa taifa leo akiwa nyumbani kwake Kigamboni, Mbutu.

Taarifa iliyotolewa na Meya wa Ubungo kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi, Nyerere alikamatwa na watu hao ambao waliambatana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbutu.
“Nimepata taarifa kutoka kwa ndugu wa Yeriko ambao wamenipigia simu alfajiri leo. Wamesema amekamatwa saa tisa usiku na watu hao ambao walivalia kiraia. Viongozi wa Chadema wanaelekea polisi kufuatilia kwa kina chanzo cha Yeriko kukamatwa,” amesema Meya wa Ubungo Jacob.
Mwanachama huyo wa CHADEMA amekuwa maarufu katika mitandao ya kijamii kupitia post zake mbalimbali za kuikosoa serikali.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment