Zitto Kabwe: Serikali inaficha makubwa katika ununuzi wa ndege

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema serikali inaficha jambo kuhusu ununzi wa ndege Boeing 787-8 Dreamliner. huku akitolea ufafanuzi juu ya ndege hizo kuwa ndege hizo ziliundwa 2009.

Zitto ametolea ufafanuzi katika ukurasa wake wa Facebook, akiandika;
Serikali inaficha jambo kuhusu Dreamliner 787-8
Tunaambiwa kwamba Ndege tunayonunua Boeing 787-8 Dreamliner Ndio kwanza inaundwa. Sio Kweli. Ndege hiyo iliundwa mwaka 2009 na kinachofanyika Sasa ni kubadilisha Injini yake Kwa sababu Injini za ndege hizo zilikuwa na matatizo ya kuwaka moto ( imetokea Kwa Ethiopian na Nippon Air ya Japan ). Hivi sasa kuna ushindani mkubwa kati ya Kampuni ya GE ya Marekani na Kampuni ya Rolls Royce Uingereza kuhusu nani apate biashara ya injini hiyo.
Hata hizi Bombardier tulizonunua hazikuundwa baada ya sisi kuweka order. Ndege hizi ziliundwa mwaka 2014 na zilikuwa tayari zimenunuliwa na Kampuni ya ndege ya Kazakhstan kabla ya baadaye kuuziwa sisi. Ushahidi wa hili ni rahisi Sana, ukipanda ATCL Bombardier tafadhali soma maandishi madogo dirishani utaona S/N 0001519017-040 DATE 10/2014. Hiyo 10/2014 ni Oktoba, 2014.
Serikali inaficha jambo katika suala la ununuzi wa Ndege hii ya Dreamliner. Serikali inajua kuwa imenunua Terrible Teen Kwa bei kubwa kuliko ilivyostahili. Shirika la ndege la Boeing linajua kuwa wametupiga bei ya kuruka na kutudanganyia Kwa kubadili injini. Serikali inajua kuwa haikusimamia maslahi ya Taifa katika mazungumzo kuhusu bei. Bahati mbaya Sana mazungumzo hayo yalimhusisha Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Fedha James Doto peke yao. Hapakuwa na Government Negotiation Team Kama ilivyo kawaida ya manunuzi makubwa ya namna haya.
Shirika la Boeing wametumia uzoefu wetu mdogo kutupiga na Ni wajibu wa Watanzania wote Kwa kutumia mahusiano yetu yote duniani kuwataka Boeing wawajibike kwa udanganyifu wao kwetu. Boeing wanapaswa kurudisha sehemu ya Fedha yetu. Ni aibu Kwa Kampuni kubwa Kama Boeing kuiibia Nchi masikini Kama Tanzania. Watanzania mnakumbuka sakata la Radar? Hii ni kurushwa zaidi ya radar. Hela zetu zirudi tujenge Reli au kuongeza Ndege.
Zitto Kabwe
Na Emmy Mwaipopo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment