ACACIA waikataa ripoti ya pili ya makinikia

Baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya pili ya mchanga wa madini (Makinikia) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli hatimae Kampuni ya uchimbaji Madini ya Acacia, imezikataa taarifa zote zilizotolewa katika ripoti hiyo ya kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya mchanga wa Madini yaliyozuiwa.
Taarifa kwa umma iliyotolewa leo (Jumanne) imeeleza kuwa kampuni hiyo inafanya shughuli zake kwa kiwango cha juu na kwa kufuata sheria za nchi huku kampuni hiyo ikitaka uchunguzi huru wa ripoti ya kamati ya kwanza na ya pili zilizoundwa na Rais Magufuli kuchunguza upya mchanga huo.
Soma taarifa kamili hapa PRESS RELEASE

“Migodi yetu inafanya kazi kihalali, kwa kufuata sheria za Tanzania, hata usafirishwaji wa mchanga huo unafanywa kwa kufuata sheria na kupata kibali cha usafirishaji,” imesema taarifa hiyo.
Kwa upande mwingine taarifa hiyo imeeleza kuwa zuio la kusafirishwa mchanga huo haliiathiri ACACIA pekee bali maisha ya maelfu ya Watanzania waliyoajiliwa na Kampuni hiyo .
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.