Account yako imeshawahi kudukuliwa ‘hacked’? Hiki ndio hutokea

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii bila shaka umewahi ama kukutana au kusikia neno ‘Hack‘ kwa maana ya kudukua account za mitandao ya kijamii ambapo mara nyingi watu maarufu ndiyo wamekuwa wahanga wa wadukuaji/udukuzi.

Ayo TV na millardayo.com zimekutana na MxCarter ambaye ni mtaalamu wa mambo ya mitandao na miongoni mwa mambo ambayo ameyatolea ufafanuzi ni pamoja na namna inavyotokea mtu akadukuliwa account yake na nini kifanyike ili usidukuliwe.
>>>”Kuna njia nyingi za ku-hack (kudukua) hizi account, na kwa hapa Bongo wanatumia njia rahisi. Mara nyingi huwa nawaelekeza hawa mastaa maana wao ndio account zao huwa zinafuatiliwa sana. Hawa hackers (wadukuzi) wanaweza kukutumia e-mail inayoonekana. Kama Instagram ndio wametumia na ukibonyeza tu ile link unakuwa umeshapatikana.
>>>Ukitumiwa e-mail inatakiwa ujue inasemaje kabla ya kufungua link…mtu kutoka Instagram hawezi kukuuliza Password yako. Tusipende pia kuweka password zinazohusiana na maisha yetu kama jina lako, mtoto wako, mahali ulipozaliwa n.k. kwa sababu inakuwa rahisi mtu kukisia password yako.” – MxCarter.
Pamoja na hayo MxCarter ameeleza mengi zaidi juu ya hatua mbalimbali zinazofanywa na Wadukuzi wa accounts mbalimbali na namna ya kujikinga nao ambapo unaweza kuyasikiliza maelezo yote kwa kubonyeza PLAY kwenye VIDEO hii hapa chini>>>


Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.