Alichokiandika Mo Dewji baada ya kukutana na Bill Gates

Tajiri kijana namba moja kwa Afrika, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya METL amefanikiwa kukutana na tajiri namba moja duniani, Bill Gates na kufanikisha moja ya ndoto zake ambapo wameweza kubadilishana mawazo juu ya biashara zao.

Dewji na Bill ambaye ni Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, wamekutana wiki hii katika mkutano mkuu wa Giving Pledge. kupitia mitandao ya kijamii, Dewji ameonekana kufurahi zaidi baada ya kukutana na tajiri huyo namba moja duniani.
“Ninafarijika na kuhamasika kujifunza kutoka kwa #BillGates hasa leo kwenye mkutano mkuu wa #GivingPledge, pia kupata maarifa juu ya namna ya kuboresha maisha ya wahitaji duniani,” ameandika katika mtandao huo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment