AT ABAINISHA MAKOSA YA WANAOMSHINDANISHA ALI KIBA NA DIAMOND

Mfalme wa miduara nchini Tanzania AT amebainisha tofauti kubwa ya kimuziki kati ya mastaa wa muziki wa bongo fleva ambao ni Ali Kiba na Diamond Platnumz.

Akizungumzia Chanzo cha sura kutoelewana na hali joto ya ushindani iliyopo kati yao AT amesema kuwa wasanii hao ni wenye umaarufu na wenye tofauti kubwa kimuziki hata kubainisha kuwa watu wanakosea kuwshindanisha wawili hao.

“kwa upeo wangu nafikiri watu wengi sana wanakosea kumshindani Diamond na Ali Kiba. Kwasababu Diamond anaimba Mass Choir , Ali Kiba anaimba Bayat…Ali Kiba officially artist na Diamond ni entertainer…ni kwamba Mass Choir ni mtu ambaye anayeimba kitu ambacho mwingine yeyote anaweza kufanya…lakini anavyoimba Ali Kiba ni vigumu sana kuweza kumuiga anachofanya” Alisema AT kupitia XXL ya Clouds Fm.
Hata hivyo AT ameongeza kuwa mfumo huo wa wawili hao kufanya muziki ni njia zinazokubalika kibiashara hivyo watakao jaribu kuwalinganisha hawatapata wanachokitafuta kwa wawili hao.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.