BARAKAH THE PRINCE: NAJ AMENIFANYA KUWA MWANAUME BORA

Ukitaja couples maarufu kwenye muziki hapa Tanzania, huwezi kuacha kuitaja ya Barakah The Prince na Naj. Wawili hao wameendelea kuwa imara kama kisiki cha mpingo na kupitia Chill na Sky, Barakah amefunguka kuhusiana na jinsi Naj alivyo msichana na tofauti na aliyefanikiwa kumbadilisha.“Naj ni yule mwanamke ambaye mimi nilikuwa namtaka,” amesema. “Unajua Naj ukimuona unaweza ukamchukulia demu fulani sister duu sana au mwanamke wa mjini kwa kumwangalia. Najma kanishangaza sana, tofauti sana na watu wanavyomfahamu. Ni fighter, ni mtu ambaye yuko in future sana yaani kila anachokifanya kwenye maisha yake ni kwaajili ya future yake,” ameongeza

“Ni mshauri wangu mkubwa sana, kaweza kunibadilisha sana mimi, kitabia kila kitu kaweza kunibadilisha. Ni vigumu sana kumwacha mtu wa hivyo tena pasipo na sababu.”

Barakah amesema hawajawahi kuachana zaidi tu ya kukosana kwa siku chache kitu ambacho anaamini hutokea kwa couples zote
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.