Bongo Movie waja na filamu ya Rais Magufuli

Kundi la filamu la Mkoa wa Shinyanga lifahamikanalo kama “Bongo Movie Shinyanga’ wameandaa filamu fupi  itakayo lenga kumpongeza Rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua anazozifanya katika kulinda rasilimali za nchi.

Kupitia Mwenyekiti wa kundi hilo Juma Songoro ameeleza kuwa “Mkoa wa Shinyanga wanampongeza Rais na wameaanda filamu fupi ambayo ni zawadi kwenda kwa Rais kwa jitihada anazozichukua katika kulinda rasilimali za nchi ikiwemo madini.”
Filamu hiyo fupi imepea jina la ‘Tanganyika karne ya 18’ na inaonyesha nchi za nje jinsi wanavyoiba madini kutoka Tanzani.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment