CALISAH: NINABANIWA KWENYE FASHION INDUSTRY SABABU NILIGOMA KUTEMBEA NA MADESIGNER MASHOGA

Model wa Tanzania, Calisah, amesema kitendo cha kukataa kutembea na madesigner mashoga na wenye majina makubwa Tanzania, kilipelekea kubaniwa fursa zote za modelling, kitu ambacho amesema hakimwathiri kwa chochote.

Akizungumza kwenye kipindi cha Chill na Sky, Calisah amedai kuwa watu hao walitaka wamweke kwenye himaya zao ili atimize haja zao, lakini baada ya kuwakataa, walimchukia na kuanzisha vita naye. Ameongeza kuwa sababu ya tasnia hiyo kutofanikiwa, ni laana kubwa iliyoigubika kutokana na vitendo vya ushoga.
“Wale wakiwa hawakupendi, huwezi kutoka,” amesema. “Uwe na hela labda au uwe na jina, au uwe na connection tayari za nje,” amesema. Baada ya kuwakataa, watu hao walianza kumtenga kwenye kazi zao.
Calisah ameeleza kuwa siku zote watu hao hutafuta vijana wapya, wakimaliza shida zao huelekeza macho yao kwa vijana wengine. Ameongeza kuwa kitu kilichokuza zaidi bifu kati yake na wao, ni baada ya kuwatukana mtandaoni na kuwataja majina.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment