Diddy aongoza orodha ya mastaa waliolipwa fedha nyingi 2017

Sean ‘Diddy’ Combs ni kama mwanaga kwenye giza. Rapper huyo ametajwa na jarida a Forbes kuwa ndio mtu maarufu anayeongoza kulipwa fedha nyingi zaidi kwa mwaka huu.
Rapper huyo ametajwa kulipwa kiasi cha dola milioni 130 kwa miezi 12 iliyopita. Beyonce anafuata kwenye orodha hiyo akiwa amelipwa dola milioni 105.
Wakati huo huo Taylor Swift aliyeongoza rodha hiyo kwa mwaka jana kwa kulipwa kiasi cha dola milioni 170 ameporomoka mpaka katika nafasi ya 49 akiwa amelipwa dola milioni 44 kwa mwaka huu. Hii ni orodha ya mastaa 10 wanaoongza kulipwa zaidi.
1. Diddy, $130 million
2. Beyoncé, $105 million
3. J.K. Rowling, $95 million
4. Drake, $94 million
5. Cristiano Ronaldo, $93 million
6. The Weeknd, $92 million
7. Howard Stern, $90 million
8. Coldplay, $88 million
9. James Patterson, $87 million
10. LeBron James, $86 million
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment