Ebitoke alegeza ‘Ben Pol akinikataa basi maana watu wanaongea sana’

Mchekeshaji wa Timamu Media, Ebitoke amedai kuna maneno mengi yamezuka baada ya yeye kutangaza kwamba anampenda muimbaji Ben Pol na angependa aolewe naye.

Ebitoke amedai sio kwamba maisha yake hayataendelea kama muimbaji huyo akikataa ombi lake kama baadhi ya watu wanavyodai katika mitandao ya kijamii.
“Napenda watu waelewe kitu kimoja, mimi sijampenda Ben Pol kisa nimpe bikra yangu,” Ebitoke aliliambia gazeti la Mtanzania. “kwa mfano akikataa kunioa basi nitamwacha aendelee na familia yake, kwa sababu watu wanaongea kinoma, lakini kuhusu hilo nitaendelea kujituza mpaka mwanaume wa kweli atokee kwenye maisha yangu ndiyo nitampa bikra yangu.
Mapema wiki hii mchekeshaji huyo alidai kama muimbaji huyo akikataa ombi lake basi atajiua.
Ben Pol alisema anaheshimu hisia na mchekeshaji huyo huku akidai kwa sasa yupo kwenye mahusiano.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment