Gabo Zigamba alizwa na ‘Magabo feki’

Gabo Zigamba ameonyesha kuumizwa na watu wanaotumia jina lake kujipatia fedha kupitia mitandao ya kijami.
Mastaa wengi wamekuwa wakikutana na balaa hilo – Lakini sasa janga hilo limeonekana kumuandama sana muigizaji huyo wa filamu hapa Bongo hadi kufikia hatua ya kushindwa kuvumilia na kuamua kufunguka kupitia mtandao wa Instagram.

Kupitia mtandao huo Gabo ameandika, “Jamani watanzania mbona mnafanya hivii 😢😢 kwanini lakini Tunachafuana? Huu ni utapeli umekuwa ukiendelea kila mara na sasa umeshika kasi na nguvu.”
“Gabo hawa wasiokuwa mimi wamekuwa ni wengi mno huku wakiwatapeli watu kwa nafsi ya kuuza bidhaa mbalimbali au Kudhulum kwa mifano hii tafadhari tabia hii ikome… #GentlemanVibe,” ameongeza
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment