Haya ndiyo aliyozungumza Lowassa baada ya kuhojiwa na Polisi kwa saa nne

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alifika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuitikia wito wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai ‘DCI’ kwa ajili ya mahojiano ambapo amekaa takribani saa 4.

Baada ya mahojiano hayo Wakili wa CHADEMA, Peter Kibatala amesema kuwa mahojiano yalihusiana na kile kilichosemakana kuwa kuna kauli alizozitoa Edward Lowassa ambazo ni za kichochezi na ameachiwa baada ya kujidhamini mwenyewe hivyo ataripoti tena Alhamisi saa sita.
Baada ya kutoka kwenye mahojiano Edward Lowassa amezungumza na kusema:>>>Niliitwa Polisi kuulizwa kuhusu hotuba niliyoitoa siku moja kabla ya Eid, nimetoa maelezo yangu tumeelewana vizuri tutakutana tena Alhamisi saa sita. Ni mambo yanayohusiana na kuwekwa ndani Masheikh wa Kiislam.” – Edward Lowassa

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment