IRENE UWOYA ASEMA HAMCHUKII WEMA SEPETU, ASIFIA UIGIZAJI WAKE

Irene Uwoya amesema hamchukii Wema Sepetu kama ambavyo baadhi ya watu wanadhani.


“Sio kweli, kwanini nimchukue,” alisema Irene kwenye kipindi cha Chill na Sky. Hata hivyo amesema Wema na yeye hawajawahi kuwa marafiki zaidi tu ya kuwa kwenye fani moja ya filamu.

“Unajua ukizungumza marafiki unazungumza kitu kikubwa sana, urafiki ni kitu kingine, [Wema] ni muigizaji mwenzangu,” amesema.

Kuhusu uwezo wa Wema kuigizaji, Irene amesema, “Wema ni muigizaji mzuri, yuko natural na ana unique wake. Kikubwa kwenye uigizaji ukiwa unique, like ukiwa na kitu ambacho mtu mwingine hana. So yuko unique kwenye uigizaji wake, sauti yake iko tofauti na watu wengine. Kwahiyo akiigiza ukisikitia tu sauti unajua huyu ni Wema yaani hata ukiwa mbali ni muigizaji mzuri.”

Wema na Irene wamewahi kuigizaji pamoja kwenye movie ya JB, Dj Ben.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.