Isingekuwa Katiba, ningetamani Rais Magufuli aongoze siku zote – Mhe. Mwinyi

Rais Mstaafu wa awamu ya pili Tanzania, Mh Ally Hassan Mwinyi amesema kama si utawala wa Kikatiba uliopo nchini,Rais Magufuli ulipaswa kuendelea kuwa Rais wa siku zote.

Mhe. Mwinyi ameyazungumza hayo jana wakati akitoa salamu za Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja , vilivyopo jijini Dar es salaam.
“Rais wetu kaleta mambo mazuri mengi sana sana, leo nchi imetulia, leo unakwenda madukani unapata huduma nzuri , leo unakwenda hospitali unaheshimiwa, leo unakwenda ofisi yoyote ile unaheshimiwa na kupata huduma nzuri,tumepata serikali nzuri ya kuwatumikia watu,” alisema Mh. Mwinyi.
“Kwahiyo kiongozi huyu ni wa kumuenzi sana sana ni wa kumsaidia sana sana na kumsifu sana na sio kusifu kwa uongo uongo, tumsifu kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa anayofanya si kwa manufaa yake bali ni kwa manufaa ya Watanzania wote. Tumuunge mkono Rais wetu, laiti isingelikuwa katiba hafupishwi muda fulani ningeshauri huyu bwana huyu awe Rais wetu wa siku zote.”
Na Emmy Mwaipopo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment