Kila mwanamke anatamani kutoka na Diamond – Amber Lulu

Msanii na Video Queen anaekuja kwa kasi kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Amber Lulu ameweka wazi hisia zake kwa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kwa kusema kuwa yupo tayari kutoka kimapenzi na Baba Tiffah kama ikitokea.

Amber Lulu
Amber Lulu amesema kwa sasa hapa Bongo anavutiwa sana na Diamond Platnumz sio tu kwa kazi zake bali hata ikitokea wakawa wapenzi yeye yupo tayari kwani hakuna mwanamke asiyependa kuwa nae.
Kibongo Bongo sijaona mwanaume zaidi ya Diamond kwanza ana ni inspire na maisha yake yaani anajiweka kazi na kila kitu na sio kwamba na wish ku’date nae tuu bali kufanya nae kazi pia,” amesema Amber Lulu huku akisisitiza kuwa kila mwanamke ana ndoto za kuwa nae.
Kama ikitokea kutembea nae is ok….sio mimi peke yangu kila mwanamke anawish kuwa nae…kila mtu mimi naamini wachache sana ambao hawamuhitaji,” amesema Amber Lulu kwenye mahojiano yake na Times FM.
Hata hivyo mrembo huyo amesema Diamond Platumz kwa sasa ni Baba na ana familia yake hivyo hafikirii sana kuwa nae kimapenzi zaidi ya kufanya nae kolabo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment