Kilichopelekea Yamoto Band kila mmoja kuchomoka kivyake

Imebainika sababu ya kundi la Yamoto Band kuamua kila msani kutoa wimbo wake ni baada ya msanii Aslay kutoa wimbo ‘Kida’ bila ruhusa ya uongozi wa kundi hilo na bila kushauriana
 na wenzake.
Yamoto Band
Akizungumza na EA Radio katika kipindi cha Planet Bongo, msanii Beka amesema baada ya Aslay kuchukua hatua hiyo nao walishawishika kufanya hivyo ndipo walipomba ruhusa hiyo kwa uongozi na kukubaliwa kufanya hivyo.
“Kile kitu kilifanya tujiulize kwa nini huyu katoa ngoma sisi wengine tukikaa kimya tutaonekana kama hatuna uwezo wa kufanya kitu, ebu nasisi tufanye lakini hatukutaka kufanya kama alivyofanya yeye, basi tukaomba uongozi wetu na kukubaliana, Mkubwa akasema mnakuwa mnajiongeza na kujikuza kwenye muziki,” amesema Beka.
Beka ameongeza kuwa zamani watu walikuwa wanawaomba kila mmoja atoe wimbo wake lakini kwa wakati huo walishindwa kujibu maombi yao.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment