MH. MBOWE AKANUSHA KUHUSIKA KIMAPENZI NA WEMA SEPETU

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Freeman Mbowe amekanusha kuhusika katika sauti ya maongezi inayosambaa kuwa yupo katika mahusiano ya kimapenzi na Staa wa filamu ‘Wema Sepetu’.

Sauti hiyo iliyosemekana kuwa ni Wema na Mh. Mbowe ilisambaa kwa kasi kitendo ambacho Wema Sepetu alijitokeza kwa kupost maelezo katika picha kupitia akaunti yake ya Instagram na kukanusha kuwa sio yeye na inonekana wazi kuwa kuna mtu aliyehusika kuigiza sauti yake kwa lengo la kuchafua majina ya wanaohusishwa.
“mimi ninalichukulia kama taarifa za kawaida ya maji taka ambazo zinasambazwa, taarifa ambazo zinategenezwa hazina ukweli wala hazina msingi wowote ndo ambacho naweza kusema kwa sasa kwasababu hizo taarifa sio za kweli…timu yangu ya mtadao inajaribu kufatilia kujua zimeoriginate kwa nani” Amesema Mh. Mbowe katika simu na Perfect.
Hata hivyo Mbowe amesisitiza kuwa hajawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Wema Sepetu na kubainisha kuwa kwasasa hana chochote anachoweza kuzungumza kwakuwa jambo hilo liko katika mikono ya wafatiliaji ili kujua nani amehusika.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment