Mhe. Mdee na Bulaya wapigwa ‘stop’ bungeni hadi 2018

Mbunge wa Kawe,Halima Mdee na mbunge wa Bunda Esther Bulaya wameadhibiwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano wa bunge la bajeti lijalo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao. Kamati ya Maadili ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.
Wabunge hao wameadhibiwa hivyo kwa kudharau mamlaka ya Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment