Mikataba ya kiingereza ilinikwamisha – Saida Karoli

Msanii mkongwe wa muziki wa asili nchini, Saida Karoli amedai kuwa mikataba aliyokuwa akiingia na mapromota wa muziki hapo mwanzoni ilikuwa inaandikwa kwa lugha kiingereza hivyo ilimpelekea kuweza kunasa kwenye mitego mingi.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa nafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Orugambo’ amesema sababu hiyo ndiyo iliyopelekea muziki wake kupotea na yeye mwenyewe kutosikika kwa kipindi kirefu.
“Mikataba mibovu ndiyo iliyonifanya nishuke kiasi hicho. Nilikuwa nikipewa mikataba ya kiingereza wakati sikuwa nikijua kusoma wala kuandika, hivyo sikuwa nikijua kilichokuwa kikiandikwa kwenye mikataba ile,” amesema Saida katika mahojiano na gazeti la Mtanzania.
Mkali huyo kutoka Bukoba ameongeza kuwa, kwa sasa anajua kusoma na kuandika vizuri lugha hiyo [kingereza] pia anatumia Kiswahili katika mikataba yake ya sasa itakayokuwa akiingia.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment