Mimi sio mpinzani wa maendeleo – Bi Anna Mghwira

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa mkuu wa mkoa huo, huku akisema kuwa yeye sio mpinzani wa maendeleo.

Bi Anna Mghwira amesema hayo wakati wa hafla ya kuapishwa iliyofanyika leo, Jumanne jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu, kumekuwa na minong’ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo,” amesema Mghwira.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.