MR BLUE: KUOA KUMENIPUNGUZIA KIDOGO USUMBUFU TOKA KWA WASICHANA

Mr Blue amesema kuwa na mke kumemsaidia kwa kiasi fulani dhidi ya usumbufu toka kwa wasichana. Mkali huyo wa Mboga Saba, ameiambia Dizzim Online kuwa bado wasichana wanamnyelea lakini sio kama ilivyokuwa zamani.

“Ni kweli zamani nilikuwa nasumbuliwa sana na wadada wakiwa wanahitaji kuwa na mimi kimapenzi,” amesema Blue.” Lakini niseme kwamba mpaka sasa bado inaendelea ingawa haifanani na zamani, na hii nafikiri kwasababu ya mimi kuoa. Kama ambavyo tunajua ndoa ni kitu kikubwa na watu wengi wamekuwa wakiheshimu mume wa mtu, ila kama kawaida kuna wadada ambao ni wabishi, yaani hawakubali kushindwa bado tu wanaendelea kunitafuta ila ndio hivyo nishaingia kwenye ndoa,” amesisitiza.
Mr Blue na mke wake Wahyda wamejaaliwa watoto wawili, Kherry na Khairriyah.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment