Mzee Yusuf afiwa na mkewe

Aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Taarabu nchini Tanzania, Alhaj Mzee Yusuf jana usiku amefiwa na mke wake wa pili wa ndoa ajulikanae kwa jina la Chiku Khamis baada ya upasuaji (Operation) uzazi kutokwenda salama.

Mzee Yusuf akiwa na Mke wake Chiku enzi za uhai wake
Mzee Yusuf amesema mke wake alianza kuugua uchungu wa uzazi kuanzia asubuhi jana na alipoona hali yake inazidi kuwa mbaya ndipo alipochukua uamuzi wa kumpeleka Hospitali ya Amana ambako alifanyiwa upasuaji na kwa bahati mbaya mtoto akazaliwa akiwa ameshafariki na muda mfupi baadae mama mzazi nae akaaga Dunia.
Chiku Khamis ameacha watoto wawili wote wa kike na mazishi ya marehemu  yanafanyika leo saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Bongo5 Media Group tunatoa pole kwa familia ya Mzee Yusuf, pia endelea kufuatilia kwa karibu mtandao wetu ili tuweze kukujuza yatakayojiri.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment