NANCY SUMARI APONGEZA UKUAJI WA SEKTA YA MITINDO NCHINI

Kwa sasa Tanzania kumekuwepo na wanamitindo wengi ambao nao wanachangia kukuza soko la mitindo nchini huku wengine wakiwa na majina makubwa dunia nzima. Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari ambaye pia alipata taji la Miss Africa mwaka huo huo amezungumzia maendeleo ya sekta hiyo nchini.

Akiongea na Dizzim Online, Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja, Zuri, amewapongeza wanamitindo kwa hatua kubwa waliyofikia.
“Kwa Tanzania kuna wanamitindo wengi sana ambao wamejitahidi kufikia viwango vya kimataifa na wanakuwa wanafanya kazi na wabunifu wakubwa sana duniani, jambo ambalo lazima tulikubali na tuwape support sana,” amesema.
“Of course, uanamitindo sio soko kubwa sana hapa Tanzania lakini kwa nafasi zetu wamemeza kujitahidi sana, wameweza kuchangamkia fursa pia, wameweza kujiongeza, na ninaamini kadri siku zinavyoenda ndio tunazidi kufika mbali zaidi. Najua bado tasnia bado ndogo kuweza kupata kipato kikubwa lakini naamini haya yote yataisha tuendelee kukaza,” amesisitiza.
Pamoja na mambo mengine, kwa sasa Nancy ni anajihusisha na shughuli za kusaidia jamii kupitia taasisi yake ya Neghesti Sumari Foundation.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.