Natamani mume wangu angekuwa mwanaume wa kwanza… – Shamsa Ford

Mwigizaji kutoka Bongo Movie, Shamsa Ford amesema anatamani mume wake angekuwa mwanaume wa kwanza kumuonyesha katika mitandao ya kijamii na watanzania kumjua hamasa ambayo anaipata kutoka kwa mwigizaji mwenzake, Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambaye kwa mujibu wa Shamsa amekuwa akifanya maisha yake ya kimahusiano kuwa binafsi zaidi.
Kupitia mtandao wa Instagram wa Shamsa ameandika,

 “Tujifunze kusifiana tukiwa hai siyo mpaka mtu afe ndo umsifie, naomba nitumie nafasi hii kukupongeza msanii mwenzangu una vitu vingi vikubwa ambavyo wasanii wengi wa kike tunatakiwa kukuiga, la kwanza napenda bidii yako ya kufanya kazi, wewe ni mwanamke mpambanaji sana, unajituma sana kiukweli na wala hukati tamaa.
Jennifer Kyaka
“Pia ni mtu ambae hata ukipata mafanikio siyo mtu wa kujionesha na wala huna mbwembwe. Lakini kubwa kuliko vyote napenda unavyoweka mahusiano yako ya mapenzi private, sijawahi ona hata siku moja umempost sijui boyfriend na hicho ndo kitu kizuri kwa mtoto wa kike,” aliongeza Shamfa.
“Mimi kwa upande wangu ningerudisha siku nyuma kipindi kile nipo single nisingempost au kumuweka wazi mwanaume yoyote niliyekuwa naye kipindi kile. Natamani mume wangu ndo angekuwa mwanaume wa kwanza kwa watanzania kumjua, natamani wasanii wengi wa kike wangeiga mfano kwako. Misingi uliyojiwekea kwenye maisha yako ni mizuri sana dada yangu, una heshima na thamani kubwa sana. Hongera sana Jennifer Kyaka,” alifafanua zaidi.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment