Ndesamburo alikua shujaa wa mabadiliko – Mh. Lowassa

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa ameeleza kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema) na kueleza kuwa alikua shujaa wa mabadiliko.
Mh. Edward Lowassa
Ndesamburo aliyekuwa Mbunge kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 amefariki dunia ghafla leo hii wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mh. Philemon Ndesamburo
Lowassa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter ametweet, “Nimesikitishwa sana na kifo cha ghafla cha Mzee Ndesamburo, Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi natoa pole kwa familia na wote. Mzee Ndesamburo alikua shujaa wa kweli wa mabadiliko wa miaka mingi na mwenye mchango mkubwa kwenye siasa za demokrasia katika Taifa letu.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment