NINA FURAHA ZAIDI KWA KUTOUWEKA HADHARANI UHUSIANO WANGU – PENNY

Watu wengi wamekuwa wakitamani kusikia au kuona mahusiano ya mtangazaji wa TV, Penny Mungilwa. Hata hivyo ameiambia Dizzim Online kuwa ameamua kuyaweka private tofauti na ilivyokuwa enzi ana uhusiano na Diamond Platnumz.

Amesema, “Mimi kitu kimoja nilisema, kwa vile najiamini mapenzi mazuri ni yale ambayo yapo private na hata kukitokea matatizo nyinyi wenyewe mnaweza kuyamaliza. Nipo kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana na nina furaha nayo tu, lakini kwa bahati mbaya au mzuri mimi na mwenzangu tumeamua tufanye private ili yawe salama zaidi. Labda tuwafahamishe wale watu tunaowaamini yaani ndugu na marafiki zetu ikiwa official yaani nimechumbiwa ndio tutaweka kwenye hadhara, hii ni kwa usalama zaidi.”
Kuhusu uwazi wa uhusiano wake na Diamond, Penny amesema, “Sikuchukizwa, ila ninawaumiza watu wangu wa karibu kwasababu kama unavyojua kwenye mapenzi kuna kupanda na kushuka na vile vitu vilivyokuwa vinaandikwa vilikuwa vinawaumiza watu wangu wa karibu, kaka zangu dada zangu, so vile ndio vitu vilivyokuwa vinaniumiza mimi. Yale mahusiano yalikuwa ya heri, ila vitu vilivyokuwa vinasemwa kuhusu yale mahusiano ndio vilikuwa vinanikera.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment