Sioni aibu kuolewa na mwanaume niliyemzidi umri – Riyama

Muigiza wa Filamu nchini, Riyana Ally na mumewe ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Leo Mysterio wamesema hawaoni aibu kuishi pamoja kisa umri.


Wakizungumza katika kipindi cha Twenzetu cha Times FM, Riyama amesema yeye binafsi haoni aibu wala hana hofu kuolewa na mwanaume ambaye yeye amemzidi umri zaidi ya miaka saba. Kwa upande wake Leo Mysterio ameeleza wakati anataka kumuoa Riyama alisemwa sana na kukosolewa vikali.
“Eti kwa sababu umri ni mkubwa lakini kwa sababu sisi ni watu wa dini haikua kazi kumaliza swala la ndoa. Niliwahi kutoa wimbo maalum kwa ajili ya Riyama na ilinitoka moyoni kabisa kitu ambacho kiliwashangaza wengi,” amesema Leo Mysterio
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment