Tunampongeza Rais Magufuli kwa kuvunja miiko ya siasa Tanzania -ACT

Chama cha ACT-Wazalendo kimempongeza Rais Magufuli kwa kumteua aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho Anna Mghwira kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kumshauri kuwa asichoke kuteua wengine wanaofaa.

Kaimu Kiongozi wa ACT, Samson Mwingamba alizungumza na waandishi wa habari Jumatano hii alisema kuwa Rais Magufuli asisite kuja kuvuna viongozi wengine.
“Kama ya uongozi ina mpongeza muheshimwa Rais kwa kuvunja miiko ya siasa za Tanzania kwa kuanza kuteua upinzani katika utumishi wa umma, uteuzi wa mara ya pili wa ACT-Wazalendo ni kielelezo kuwa chama chetu kina watu makini na wanaofaa kuongoza,kwa hiyo Rais asichoke na asisite kuja kuvuna na wengine, maana tumeonyesha uwezo wa kutengeneza wengi wa aina hiyo,” alisema Mwigamba.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment