Wanaume wengi wana tabia ya kuchepuka – Dkt Kigwangalla

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa wanaume wengi wamekuwa na tabia ya kuchepuka sana hivyo amewaasa wanaume kuacha tabia ya kuchepukaji.

Dkt Kigwangalla ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge Suzan Lyimo alietaka kujua kwanini idadi kubwa ya wanawake ndiyo wamekuwa waathirika wa virus vya UKIMWI.
“Wanawake wanaambukizwa zaidi kuliko wanaume kwasababu uwiano hauko mbali sana tofauti ni ndogo lakini kweli kwamba maumbile ya kibailojia ya wanawake ni tofauti sana na maumbile ya wanaume lakini pia lakini tabia za wanawake kuhusiana na ngono ni tofauti sana na tabia za wanaume kuhusiana na ngono wanaume wengi wana tabia ya kuchepuka sana na mara nyingi wanaweza waka vitoa virusi nje wakavileta kwenye ndoa zao kwa wanawake ambao wametulia hilo halibishaniwi,”alisema Kigwangalla.
“Kwahiyo nitoe rai kwa wanaume wenzangu kujipanga sana kwenye eneo hili la kuchepuka kuachana na michepuko lakini pia kupima afya zetu kupima hali zetu lakini pia kupima hali za wenza wetu kwa wale ndugu zangu waislam tumepewa fursa ya kuoa hata wake wa nne, kwahiyo ni bora ukawa na wake nne kuliko kwenda kuwa na mtu usio mjua.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment