Alikiba afunguka kuhusu bidhaa zake mpya na lebo ya King’s Records

Umeshawahi kusikia ujio wa bidhaa mpya za Alikiba? Unajua ni vitu gani hivyo ambavyo anakuja navyo kwa mashabiki wake?

Basi tegemea kuona bidhaa za mavazi na vinywaji kutoka kwa msanii huyo. Alikiba amethibitisha hayo wakati alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Msetoea cha Citizen Radio, Mzazi Willy Tuva.
“Kulikuwa na tetesi hizo kuwa Alikiba ataingiza bidhaa zake sokoni lini, lakini kiukweli ipo ni kwamba tofauti na watu wengi walivyokuwa wakifikiria lakini hizo bidhaa zipo, nimeshasajili kila kitu kwa hiyo ni kuingiza tu bidhaa,” amesema Kiba.
“Plan zetu ndio zinafanyika na soon watu tutawaonyesha kuanzia chini ni kitu gani ambacho tunakifanya ili twende nao sambamba wajue bidhaa itafika lini au kama imekamilika tuwaonyesha kama imekamilika. Kila kjitu nitakjuwa nawaonyesha kama ni energy drinks, mavazi,” ameongeza.
Muimbaji huyo ameendelea kwa kuzungumzia kuhusu mipango yake ya kufungua lebo kama baadhi ya wasanii wengine wakubwa, amesema, “Mimi nilisha kuwa na lebo muda mrefu sana, sema kazi zangu hazikuwa za matangazo kama hivyo. Ni muda mrefu nimeanza kufanya muziki na kusaidia watu sio leo, toka nipo katika game kabla sijapumzika nilikuwa na lebo yangu ya muziki lakini haikuwa inatangazwa. Sasa hivi kila kitu kipo kwenye utandawazi, kila mtu anatakiwa kujua Alikiba ana lebo na anafanya hivi na hivi.”
“Nipo na wasanii ambao nimewasaini lakini bado sija watangaza wala kutoa kazi zao, tupo kwenye procsess za mwisho kwa sababu kila mtu kasharekodi nyimbo yake bado kushoot video ndio tuwatangazie watu,” amesisitiza.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment