BBC waahidi kuwafikiria watangazaji wa kike kwenye viwango vya mishahara

Baada ya kuandamwa mitandaoni kwa ulipaji mishahara isiyona uwiano, Shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), limekiri wazi kwamba linahitaji kufanya juhudi zaidi kuondoa tofauti za mishahara kwa wafanyakazi wake baina ya wanawake na wanaume
Kwa viwango vya mishahara walivyovitoa vinaonesha kuwa jumla ya mshahara wa wanaume, ni asilimia 10 zaidi ya wanawake katika shirika zima na limeahidi kuondoa hitilafi hiyo ifikapo mwaka 2020.


Taarifa hiyo imetolewa kujibu barua iliyoandikwa na Watangazaji maarufu wanawake kwenye Shirika hilo na kumtumia mkurugenzi mkuu, Tony Hall kumsihi aondoe tofauti hiyo katika malipo.

Jumatano, BBC ilichapisha orodha ya watangazaji na waigizaji wake wanaopata karibu dola laki mbili kila mwaka kufuatana na maagizo ya serikali.


Katika orodh hiyo theluthi moja ya wanawake wanalipwa kidogo sana ukilinganishwa na wanaume.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.