Dc Hapi aamuru Halima Mdee akamatwe awekwe ndani

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni kumkamata Mbunge wa Kawe, Halimamdee kwa tuhuma za kutoa lugha Chafu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dc Happy ameyasema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam.
“Mhehimiwa Halima Mdee amemtaja Rais kwa jina lake kuwa amekuwa na tabia ya ovyo kuwa na maneno ya ovyo ndo kumepelekea kufanya maneno yake kuwa sheria la pili Mdee huyu anaeleza kuwa Rais huyu huyu ataagiza tutembee vifua wazi kwamba wanawake na wamnaume tutembee vifua wazi,” amesema Dc Hapi.
“Maneno yake ni ya kichochezi ambayo hayakubaliki, hayafai kutolewa na kiongozi kama yeye hivyo namuagiza kamanda amkamate Mdee amweke ndani kwa saa 48 ili ahojiwe yale yote aliyoyaongea ili afikishwe kwenye vyombo vya usalama.”
Halima Mdee anadaiwa kutoa maneno hayo ya kukashifu na ya uchochezi katika mkutano wake wa Baraza la Wanawake Chadema uliofanyika jana.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment