Hii ni kwa wanaotumia jina la Babu Tale vibaya

Meneja wa kundi la Tip Top Connection na Diamond Platnumz, Babu Tale ameonyesha kukerwa na watu wanaotumia jina lake kufanya biashara zao katika mitandao.

Kupitia mtandao wa Instagram, Tale amewatolea uvivu watu hao kwa kuandika ”Huyu m**** anajua kunichafua jamani khaaa. Huyu mtu sio mimi kuna mpuuzi anaisi simjui naona nikimtolea uvivu ataishia kuomba samahani najua Upo mwanza endelea ila siku nikiamua utakuja ona dunia chungu.”
Mtu huyo amekuwa akitumia jina la Babu Tale katika mtandao wa Facebook ambapo amekuwa akijidi kwa kuuza mikoba. Majina na picha za watu maarufu yamekua yakitumika na baadhi ya watu vibaya katika mitandao ili kutapeli au kufanya biashara zao.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment