Kinachoendelea kuhusu Tundu Lissu toka akamatwe jana

Leo July 21,2017 ikiwa ni siku moja tangu alipokamatwa Mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu, Wakili wa Mwanasheria huyo Fredrick Kihwelo ameongea na Waandishi wa habari kuhusu kinachoendelea.

Kihwelo amesema bado Tundu Lissu anashikiliwa na Polisi licha ya kumaliza kuhojiwa tangu alipokamatwa jana na kwamba kwa sasa wapo Kituo cha Polisi kati ili kujua hatma ya Lissu kwani jibu walilopewa awali na Polisi kwamba hawawezi kusema kama atapelekwa Mahakamani ama la, halijitoshelezi.
“Tukiwa kama Mawakili wake lazima tujue kama watampeleka Mahakamani ama la, na kama hawampeleki ni nini kinaendelea wakati ameshahojiwa, leo ni Ijumaa kama asipopelekwa ina maana hadi Jumatatu”
Naendelea kufatilia zaidi na nitakufahamisha kila taarifa mpya inapotoka
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment