Mastaa na wadau wamlilia mtangazaji wa EFM, Bikira wa Kisukuma

Mastaa wa muziki, watangazaji na wadau mbalimbali wamepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Mtangazaji wa kituo cha redio cha E-Fm na Mwanamitandao ya kijamii, Seth Katende maarufu kama “Bikira wa Kisukuma” aliyefariki dunia Jumapili hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akitibiwa.

Bado ratiba ya mazishi haijawekwa wazi lakini kwa sasa msiba upo nyumbani kwa baba yake mzazi Changanyikeni Dar es salaam.
Hizi ni salamu za watu mbalimbali hukusu msiba huyo mzito.
Dina Marious
Tulikuwa wagonjwa wenza tumepishana wiki tu. Wewe umelazwa TMJ mimi nipo Sanitas kila siku lazima tuwasiliane tuchekiane vipi salama umeamkaje? kwemaa upande huo?Tupone bwana tukale firigisi,” aliandika Dina Instagram.

Simu yangu leo ilifichwa kwa muda nisielewe kinachoendelea wanaoniuguza wameuchuna mwisho ikabidi waseme tu.Kichwa kinaniuma sababu ya hali yangu lakini kimeongezeka maradufu kukulilia.Juzi unanipa moyo eti nitapona niende mtoto day Dah kumbe wewe hali imekuwa mbaya.#RIP SETH,”
Diamond
Rest in Paradise Bro… my condolences to your family and @efmtanzania ✊

Kajala Masanja
Rest in peace kaka ๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜”

Skytanzania
If u were able to see how people are sad, you wouldn’t believe. Rest in peace Seth. My condolences to the family. Amen

Clouds FM
cloudsfmtzSisi ( #CloudsMediaGroup ) tunatoa pole kwa ndugu zetu wa #EFM kufuatia msiba mzito mwanahabari mwenzetu Seth Katende ( #BikiraWaKisukuma ). Sala na dua zetu ziko pamoja na #EFM, #ETV, familia pamoja na ndugu na jamaa wa Marehemu Seth.

Mwenyezi Mungu Mtukufu aiweke roho ya marehemu mahali pepa peponi.
#RIPBikiraWaKisukuma.
Times FM
Uongozi wa Times 100.5 FM unatoa pole kwa familia ya Seth Katende (Bikira wa Kisukuma) Mtangazaji wa @efmtanzania Pamoja na @tvetanzania Katika Kipindi Hiki Kigumu Kwa Kumpoteza Mwanafamilia Mwenzetu.

Pole Kwa #EFM & #ETV, Mungu Awasimamie, Awaongoze na Kuzidi Kuwatia Nguvu Katika Msiba Huu.
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.
#RIPSeth #RIPBikiraWaKisukuma
Mkubwafellatmk
R.I.P mwanangu MUNGU kakuita sote safari ni moja inshaallah kuna siku tutakutana ila muda huu tunatakiwa tumuombee kwa MUNGU ampe kauli thabit na amuhifadhi mahala pastaiki ameen natoa pole kwa familia na ofisin kwako @efmtanzania najua mmeondokewa na kijana alio kuwa na uthubutu kwenye kazi ameeeeeeeeeen
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment