Mimi bado mjamzito, sijajifungua – Linah

Msanii wa Bongo Flava, Linah amekanusha tetesi kuwa amejifungua.

Hivi karibuni kuliibuka uvumi kuwa muimbaji huyo amejifungua taarifa ambazo Linah ameeleza kuwa si za kweli na kuwataka mashabiki wake kusubiri taarifa rasmi kutoka kwake.
“Mimi bado mjamzito, sijajifungua bado na hata mwenyewe nashangazwa na huyo mtu aliyeanza kusambaza taarifa hizo na sijui malengo yake ni yapi. Mashabiki zangu waniombee kwa sasa hivi nikiwa nakaribia kwenda kujifungua hivi karibuni ingawa siwezi kusema ni lini kwani siyo vizuri,” ameiambia EATV na kuongeza.

“Taarifa watazipata kupitia kwangu mwenyewe au kwenye mitandao yangu ya kijamii”. Tangu Linah alipoachia picha za utupu mtandaoni za kuonyesha ujauzito wake mashabiki wamekidodosa huku na kule kuja kama mrembo huyo amejifungua.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment