Mwalimu aliyechepuka na mwanafunzi kwenye maabara ‘apigwa rungu’

Mwalimu Raphael Mwape wa somo la Baiolojia katika shule ya sekondari ya wasichana ya St. Therese ya Jijini Lusaka nchini Zambia aliyedakwa June 14 mwaka huu na walinzi akifanya mapenzi na mwanafunzi katika maabara ya shule hiyo amefutwa kazi huku mwanafunzi akifukuzwa shule.


Ofisa Elimu wa Wilaya ya Kasama, Christopher Sinkamba akizungumza na Radio Mano ya nchini Zambia amesema wamefikia maamuzi hayo baada ya wananchi wengi kulalamika kuwa kuna ongezeko la Walimu kujihusisha na vitendo vya ngono na Wanafunzi wao.
Sinkamba amesema utawala wa shule ulifikisha suala hilo Polisi lakini walishindwa kumshtaki kwa tuhuma za kubaka kwa kuwa binti huyo ni zaidi ya miaka 16.
Hata hivyo Mwanafunzi huyo amefukuzwa shuleni hapo kutokana na maadili na utaratibu wa shule kwani ni shule binafsi na zina utaratibu wake.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao ni wanafunzi wenzie walioona mchezo huo ukifanyika kabla ya kutoa taarifa kwa Walinzi wamesema haikuwa mara yake ya kwanza kwa mwalimu huyo kumuingilia na kwamba siku hiyo alilazimika kufanya hivyo baada ya kushinikizwa na mwalimu huyo aliyemuita wakati akirejea bwenini.
“Mwalimu Mwape amezoea kumuita mwenzetu kila siku tukirudi mabwenini na akiwa maabara akrudi bwenini anatwambia lakini tulimueleza asikubali, lakini leo amemfungia kabisa akimtaka kimapenzi kwa nguvu wakati ana mke wake”,amesema moja ya mashuhuda na marafiki wa Mwanafunzi aliyefanyiwa kitendo hicho kibaya.
Kwa maelezo yaliyotolewa na Uongozi wa shule hiyo yanadai Mwalimu, Mwape ameoa kwa ndoa na amebahatika kupata watoto wawili.A
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment