Mwanamke mwingine Mtanzania kakamatwa na dawa za kulevya India

Mwanamke Mtanzania amekamatwa na Polisi wa Samrala, India akiwa na Dawa za Kulevya aina ya Heroin gramu 300 ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwanamke Mtanzania kukamatwa akiwa na Dawa za Kulevya kwenye Jimbo hilo.

Katika taarifa iliyochapishwa na mtandao wa The Tribune wa India, Mtanzania huyo ambaye ni Mwanamitindo anaefanya kazi zake Delhi na Mumbai alikamatwa na Polisi waliokuwa kwenye doria katika eneo liitwalo ITI-Samrala.


Baada ya kukamatwa alikutwa ameshikilia paketi ya biskuti na baada ya kuwaona Polisi alianza kula biscuits hizo lakini Polisi walipomfikia na kufungua paketi waligundua ni dawa za kulevya aina ya heroin.
Katika uchunguzi wa awali Mwanamke huyo alieleza kuwa alisafiri kutoka Delhi kuuza dawa hizo kwa mtu aliyeishi Ludhiana, tayari amefunguliwa mashtaka na atafikishwa Mahakamani.

Mwanamke Mtanzania anayedaiwa kukutwa na Dawa za Kulevya India (wa pili kushoto) akiwa na Maafisa wa Polisi wa India

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment