Mwanamuziki Shaban Dede afariki dunia

Mwanamuziki mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia leo saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Dede ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi alilazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu, Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Mbagala Jijini Dar Es Salaam, Hayo yamebainishwa na Mwanae Hamad Dede.
Marehemu atakumbukwa kwa muziki wake pamoja na utunzi aliokuwa akiufanya katika bendi mbali mbali kama vile Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park, Msando Ngoma ambako alikuwa akifanya kazi ya muziki hadi umauti kumkuta.
Historia ya Marehemu;
Shabaan Dede alizaliwa Mkoa wa Kagera mwaka 1954 ambako alianza kupenda muziki na bendi yake ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa ni ya TANU ambayo makazi yake yalikuwa Biharamulo, mjini Bukoba.
Mnamo mwaka 1979 alijiunga na bendi ya Msondo wakati huo ikijulikana kama JUWATA JAZZ  ambako alidumu  mpaka mwaka 1982 , Baada ya kutoka bendi hiyo alihamia Mlimani Park Orchestra wana SIKINDE ambako alikaa kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Bendi ya Bima a.k.a BIMA LEE.
Mnamo  mwaka 1987 Deded alirudi tena Msondo ambako alikaa  kidogo na baadaye akahamia tena Sikinde. Hata hivyo mwaka 20111 akarejea tena Msondo ambako yuko hadi umauti unamkuta.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment