Namshukuru Mungu sikufikia hatua ya kujiuza – Saida Karoli

Msanii wa muziki wa asili Bongo, Saida Karoli amesema licha ya yeye kushuka kimuziki hakufikia hatua ya kujiuza.

Saida ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Orugambo’, ameeleza licha ya kuepuka hilo hata unywaji wa pombe alisitisha.
“Vitu vingi nilipitia ila namshukuru Mwenyenzi Mungu sikufikia hatua ya kusema najiuza, na mpaka mtu anafikia anaona yeye sio kitu anaenda kujiuza barabarani, kuuza mwili wake lakini mimi sikufanya hivyo,” Saida ameiambia Power Breakfast ya Clouds FM na kuongeza.
“Nilikuwa nakunywa pombe sana lakini kutokana na kushuka kwangu nikaona na pombe niache tangu mwaka 2006, situmii bia, situmii Sigara namshukuru Mwenyenzi Mungu amenipa ustahimilivu nimesimama wima hatimae nimerudi Saida yule yule,” amesistiza.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment