Ndege iliyowapeleka majeruhi wa Lucky Vicent Marekani kuwarejesha nchini

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa ngege aina ya DC 8 itawarudisha Tanzania watoto Doreen, Saidia na Wilson mwezi ujao kama ilivyoondoka nao nchini.
Mhe. Nyarandu ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii leo kutoa taarifa hizo huku akisema kuwa wameshakubaliana na ndege hiyo kama walivyoondoka nao nchini itawarejesha na vifaa kwaajili ya hospitali hapa Tanzania.

Breaking:-NDEGE aina ya DC 8 inayomilikwa na @samaritanspurse KUWARUDISHA #Tanzania watoto Doreen, Sadia, na Wilson mwezi ujao. TUMEKUBALIANA kuwa ndege hiyo iwarudishe nchini WATOTO kama walivyoondoka, na kurejea na VIFAA kwa ajili ya hospitali hapa #Tanzania🇹🇿NITATOA ratiba kamili yenye tarehe na saa ya kuwasili (ETA) kwa watoto wetu uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mara taratibu zitakapokamilika. Asanteni wote kwa kuendelea kuwakumbuka katika Sala na dua zenu.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment