Rais Magufuli kunyanga’nya viwanda anavyomiliki Mbunge wa CCM

Rais Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka watu wote waliobinafsishiwa viwanda mbalimbali katika Mkoa wa Morogoro kuvirejesha serikalini akiwemo Mbunge wa CCM mkoani humo.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi wa Morogoro katika eneo la Msamvu jana kumueleza kero ya kunyanyaswa na Manispaa ambao wamekuwa wakiwafukuza katika maeneo wanayofanyia biashara.
“Ninarudia wito wangu niliokwisha kuutoa huko nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, na leo nataja akiwemo Mbunge wa hapa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), narudia akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM ambaye alibinafsishiwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha avirudishe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu,” alisisitiza Rais Magufuli.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment