Rihanna kurejea Afrika mwaka huu

Msanii wa muziki, Rihanna amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron, jijini Paris kwa ajili ya kutoa misaada kwa Bara la Afrika katika elimu.

Akizungumza na waandishi masanii huyo amelezea mipango yake ya kusaidia katika elimu kupitia tasisi yake. “Nilikuwa na kikao kizuri na Rais wa Ufaransa na mkewe.Wamenikaribisha na tumeongea kuhusu mada ya elimu tutatangaza tuliyoyafikia ifikapo Septemba mwaka huu,” amesema Rihanna.
Pia mrembo huyo ametangaza kurejea Afrika ifikapo Oktaba mwaka huu, kwa ajili ya kuendelea na mipango yake ya kusaidi Bara hilo katika elimu.
Mwezi wa pili  mwaka huu, msanii huyo alitunukiwa tuzo ya ‘Humanitarian of the Year’ na chuo cha Harvard kwa mchango wake katika elimu na afya.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.