Rooney atua Bongo na kikosi kizima cha Everton

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere huku kikosi hicho kikionekana kusheheni wachezaji wake nyota akiwemo Wayne Rooney.


Rooney akipanda basi muda mchache baada ya kuwasili
Wenyeji hao wa Goodson Park wamepokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudi mchezo huo na huku akizihasa timu za Tanzania kujifunza kutoka kwa wageni hawa.
Everton imewasili Tanzania kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya mchezo unaotarajiwa kuchezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi ya wiki hii.
Kivutio kikubwa katika mapokezi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza ni wananchi wengi waliojitokeza kumshabikia Wayne Rooney.











Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment